Kuna mwanamke alitaka kumloga mumewe. Akaenda kwa mganga akaambiwa nitakufanyia dawa lakini lete ndevu 3 za simba dume kisha ntakufanyia dawa mume wako atakusikiliza wewe tuu.
Yule mwanamke akasema nitazipata wapiii ndevu za SIMBA, mganga akamwambia kama hutaleta hakuna litakalokua.
Akaenda porini na manofu ya nyama akamuelekea Mungu na kumuomba huku amekaa juu ya mti akimrushia simba nofo moja baada ya jengine, ilipotimu wiki, yule simba akazoea, akawa anashuka kidogo kidogo mpak mwisho akawa karibu ya simba mpak akawa anaweza kumshika huku anamtupia vinyama.
Na hatimaye alizipata ndevu zaidi ya 3. Akaenda tena kwa mganga na kumkabidhi ndevu 3.
Alipofika mganga alishtuka hakuamini kama kaja nazo, kazipata kweli!! ilibidi amuulize ulitumia njia gani kupata hizi ndevu
Akamfahamisha tricky aliyoifanya basi mganga akamwambia dawa ya mumeo kutulia akakuskiliza na akafata unachotaka unayo bila mimi kukufanyia kitu.
Maana uliwezaje kumlagai simba mpaka akawa karibu na wewe ukazipata ndevu kisha ukashindwa kumlagai mumeo akawa karibu na wewe?
Mwanamke mwenyewe alijishangaa akarudi kwa mumewe na kujua dawa anayo mwenyewe si mganga.
Hakika mganga hana nafasi katika maisha yako, hata jambo liwe kubwa mnoo, Muelekee Mungu huku ukiwa na jitihada ya kufanikiwa nalo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment