August 13 2016 Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 ilianza rasmi kwa michezo saba kupigwa katika viwanja tofauti tofauti nchini England, kwa upande wa Ligi Kuu Englandmsimu huu unatabiriwa kuwa ni msimu wa ushindani zaidi kuliko misimu kadhaa iliyopita kutokana na kuwasili kwa makocha wenye mvuto kwa mashabiki.
Miongoni mwa michezo iliyochezwa leo ni mchezo kati ya Hull City dhidi ya bingwa mtetezi wa kombe hilo Leicester City, mabingwa hao watetezi wakiwa ugenini leo August 13 wamekubali kipigo cha goli 2-1, magoli ambayo yamefungwa na Adama Diomandedakika ya 45 na Robert Snodgrass dakika ya 57 baada ya wao kufunga goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati kupitia Riyad Mahrez dakika ya 47.
0 comments:
Post a Comment