Comments


BEI YA PILIPILI MANGA YAPANDA

WAKULIMA wa pilipili manga katika Halmashauri ya wilaya ya Muheza wameanza kupata faida kutokana na bei ya zao hilo kupanda mara dufu kutoka Sh 4,000 hadi Sh 24,000 kwa kilogramu mwaka huu.
Hatua hiyo imetokana na hatua ya wakulima kushirikiana na uongozi wa halmashauri kuweka sheria ndogo na kuwadhibiti wakulima waliokuwa wakiziuza pilipili manga kabla ya kukomaa. Ofisa Kilimo wa kata ya Tongwe, Subira Mmbago amebainisha hayo alipozungumza na mwandishi wa gazeti hili alipotembelea kijiji cha Tongwe.
Alisema baadhi ya wakulima wenye tamaa ya kupata fedha za haraka kwa makusudi waliamua kuharibu soko la pilipili manga kwa kuzivuna kabla ya muda wake na kisha kuzivundika (kupepea) ndani ya chombo chenye maji ya moto ili kutengeneza rangi nyeusi kuzifanya ziwe na rangi ya pilipili manga zilizokomaa.
Alisema kitendo hicho kiliwaudhi wanunuzi wa zao hilo hasa waliokuwa wakitoka nje ya nchi na kushusha bei kufikia Sh 4,000 kwa kilo tofauti na ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita.
Alisema pilipili manga zilizofanywa hivyo zilionesha kunyauka baada ya siku saba na kuanza kupukutika zenyewe kama unga tofauti na inayokomaa mtini kabla ya kuvunwa.
Naye mmoja wa wakulima wa zao hilo, Mariamu Mhando, wa kijiji cha Kisiwani, alisema baada ya wapepeaji kudhibitiwa mwaka huu hali imeanza kubadilika na bei imepanda kufikia Sh 24,000. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, kata zinazojihusisha na kilimo cha viungo kikiwemo cha pilipili manga ni Tongwe, Kisiwani, Amani na Magoroto.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system