Comments


MREMA MATEJA WAPELEKWE HOSPITALI

MWENYEKITI wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustine Mrema ameshauri waathirika wa dawa za kulevya kupelekwa hospitalini kupata tiba badala ya polisi kuwakamata na kuwapeleka mahabusu au gerezani ambapo huko hujazana bila kupata msaada wowote.

Aidha, amesema atamwomba Rais John Magufuli kumrejesha kazini Mwalimu wa Sekondari, Emmanuel Roman ambaye alifukuzwa kwa ajili ya utumiaji wa dawa hizo, lakini hivi sasa ameacha baada ya kupata tiba na ushauri nasaha.mremaMrema alitoa ushauri huo jana Dar es Salaam alipokutana na waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya katika Ukumbi wa Friends Corner, Manzese katika Manispaa ya Kinondoni.

Alisema anapopelekwa gerezani mtumiaji wa dawa za kulevya atakuwa hajasaidiwa, kwani atazidi kuharibikiwa badala ya kurekebishwa.

“Ni marufuku kukamata vijana wadogo wanaotumia kete. Sio kama nahamasisha waendelee kutumia ila wakikamatwa wapelekwe hospitali za Muhimbili, Mwananyamala na Temeke ambako kuna vituo vyao.

“Ukianzisha operesheni ya kukamata wezi bila kujua historia zao inawezekana ni waathirika wa dawa za kulevya, ambao wanapoanza kutumia kuacha ni kazi sana hivyo wanalazimika kuiba ili wapate hela ya kununua dawa hizo,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system