Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin amesema kuwa anahofia wachezaji hao wanaweza wasiweze kuingia Cardiff ambapo mchezo wa fainali wa UEFA mwaka huu utafanyika kwenye uwanja wa Principality Stadium mwezi Juni iwapo tu watafanikiwa kufuzu.
Hata hivyo itakuwa kama maajabu Barcelona kuingia kwenye fainali ya mwaka huu ya mwezi Juni kwani tayari wameshafungwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 dhidi ya Paris Saint-Germain.
Mapema msimu huu, beki wa PSG, Serge Aurier alinyimwa ruhusa ya kuingia Uingereza kwenye mchezo dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates mwezi Novemba kutokana na kuwepo kwenye rufani ya kesi ya kudhuru.
Lakini pia hali ya kisiasa inayohusu mpango wa Brexit ikiendelea kuwepo, Ceferin anaamini kuwa England itakumbana na tatizo kubwa kwenye mpango wa kutaka kuandaa mashindano ya Mataifa ya Ulaya mwaka 2028 au kombe la Dunia mwaka 2030.
0 comments:
Post a Comment