Comments


ALLEGRI ACHEKA KWA MADAHA TETESI ZA KUIFUNDISHA BARCA..............


Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri amezicheka habari zinazomhusisha na kibarua cha Barcelona ifikapo mwisho wa msimu huu.

Allegri ndilo jina la hivi karibuni kuhusishwa na kibarua cha Camp Nou, lakini amekanusha vikali tetesi hizo akisisitiza hazina ukweli

Tetesi kuhusu mustakabali wa kocha wa sasa wa Barca Luis Enrique zimekuwa kwa kasi kipindi chote cha kampeni za msimu huu, na mkataba wake ukitarajiwa kuisha mwisho wa msimu huu na ripoti zimedai kuwa kiwango duni cha timu kinaweza kumlazimu kuondoka.

Allegri ndilo jina la hivi karibuni kuhusishwa na kibarua cha Camp Nou, lakini akiwa ametoka tu kuzima habari za tetesi kuwa angetua Arsenal, Muitaliano huyo amesisitiza kuwa hakuna ukweli katika tetesi hizo.

"Najifunza Kiingereza na Kihispaniola? La! nilipata tabu kujifunza Kiitaliano shuleni! Nimejifunza Kitorino hapa na nimekijua vema," aliwaambia maripota.

Allegri ameshinda mfululizo taji la Serie A akiwa na Juventus na anataka kufuata nyayo za mtangulizi wake Antonio Conte kwa kutwaa mara ya tatu.
Share on Google Plus

About Unknown

1 comments:

  1. A review of The Buffet at The Wynn, NV - Dr.MCD
    I had a great time 의정부 출장마사지 on The 평택 출장샵 Buffet at the Wynn when I was staying in Vegas. It was definitely the best 영주 출장안마 buffet I've 속초 출장마사지 ever had. The food was 영천 출장안마 delicious.

    ReplyDelete

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system