Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jumla watu 574 wamejitokeza kuhakiki wa silaha zao ikiwa ni agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Makonda alitoa siku 90 kwa wakazi wa Dar es Salaam wawe wamehakiki silaha zao ifikapo Julai mosi, ikiwa ni miongoni mwa mikakati yake ya kupambana na uhalifu uliokithiri.
Kamanda Sirro alisema wanaendelea kuwahimiza wananchi waendelee kujitokeza kuhakiki silaha zao kwa muda uliotolewa kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoshindwa kuhakiki.
Hatahivyo siku za hivii karibuni, Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk John Magufuli alihakiki silaha zake anazomiliki.
<
0 comments:
Post a Comment