Comments


PATASHIKA NGUO KUCHANIKA JUMAMOSI EL CLASICO,,BBC VS MSN





ELCLASICO-APR1JUMAMOSI Aprili Mosi huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain, ipo Mechi kubwa ambayo Siku zote hubatizwa ‘El Clasico’, ikimaanisha ni Mechi ya kipekee ya hali ya juu kabisa, katika ya Mahasimu FC Barcelona na Real Madrid.

Mechi hii ni ya La Liga na inazikutanisha Barca ambao ni Mabingwa Watetezi wa Ligi hiyo wakiongoza kwa Pointi 10 mbele ya Timu ya 3 Real huku Mechi zikibaki 8.

Timu ya Nafasi ya Pili ni Atletico Madrid ambao wako Pointi 9 nyuma ya Barca na Pointi 1 mbele ya Real.

Hii ni El Clasico ya pili Msimu huu baada ile ya kwanza ya La Liga huko Santiago Bernabeu kumalizika kwa Real 0 Barca 4.

Lakini hii ni El Clasico ya kwanza kwa Meneja wa Real, Zinedine Zidane, ambae alitwaa wadhifa baada ya kutimuliwa Rafa Bemitez Mwezi Desemba.

LALIGA-TOP-MAR29Kazi kubwa kwa Zidane ni kusaka njia ya kuwazuia Washambuliaji Mtu 3 za Barca, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, ambao wamebatizwa MSN, na ambao kati yao wamefunga Jumla ya Mabao 69 kwenye La Liga.

Lakini wenzao wa Real, Gareth Bale, Karim Benzema na Cristiano Ronaldo, wakijulikana kama BBC, wamefunga Bao 63 za La Liga huku Ronaldo ndie akitamba kuwa Mfungaji Bora wa Ligi hii akiwa na Mabao 28.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

Barcelona (Mfumo 4-3-3): Bravo; Alves, Pique, Mascherano, Alba; Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, Suárez, Neymar

Real Madrid (Mfumo 4-3-3): Navas; Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo; Modric, Isco, Kroos; Benzema, Bale, Ronaldo

LA LIGA

Jumapili Machi 20

Ratiba

**Saa za Bongo

Ijumaa Aprili 1

2130 Rayo Vallecano v Getafe CF

Jumamosi Aprili 2

1700 Atletico de Madrid v Real Betis

1915 Las Palmas v   Valencia C.F

2130 FC Barcelona v Real Madrid CF

2305 Celta de Vigo v Deportivo La Coruna

Jumapili Aprili 3

1200 Athletic de Bilbao v Granada CF

1600 Malaga CF v RCD Espanyol

1815 SD Eibar v Villarreal CF

2030 Sevilla FC v Real Sociedad

Jumatatu Aprili 4
2030 Levante v Sporting Gijon

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system