Comments


MVUA ZA MASIKA ZATARAJIWA KULETA MAFURIKO

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za masika katika ukanda wa Pwani, zinazotarajiwa kuanza wiki hii, zitakuwepo kwa vipindi vifupi na zitakuwa kubwa zitakazoweza kusababisha mafuriko.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi amesema pia  hali ya joto kali itaendelea kuwepo nyakati za usiku huku ikipungua nyakati za mchana.
“Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa wakati wa msimu huo wa masika na kuweza kusababisha hata mafuriko, ni vema wananchi kufuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa vipindi vifupi,” alisema Dk Kijazi.
Mvua za masika zimeanza kama ilivyotabiriwa huku ukanda wa Pwani zikianza wiki ya kwanza ya mwezi Aprili.
Dk Kijazi alisema ingawa maeneo hayo ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, yanaonesha kuwepo mvua za wastani hadi chini ya wastani, lakini mabadiliko ya hali ya hewa yanafanya kuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system