Iwapo Athanas atendelea na kiwango alichoonyesha dhidi ya JKT Ruvu, ni dhahiri kibarua cha Laudit Mavugo kitakuwa hatarini
Pastory ameiambia Goal, kuwa ametua Simba kikazi na atahakikisha anaitumia vizuri nafasi hiyo ya kucheza kikosi cha kwanza kwa kuisaidia timu yake kuweza kutwaa ubingwa kama ambavyo wamekusudia.
“Najua siyo kazi rahisi lakini nitajitahidi kuhakikisha nacheza kwa juhudi kwenye mazoezi na hata mechi ili kocha aendelee kunitumia kwenye kikosi cha kwanza ,” amesema mshambuliaji huyo.
Mkali huyo mwenye historia ya kuifunga Yanga, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu, alisema anajua Simba kuna wachezaji wenye uwezo na majina makubwa lakini atajitahidi kupambana ndani ya uwanja ili kudumu kwenye kikosi cha kwaza.
Alisema analichukia benchi na hayupo tayari kukaa benchi ndiyo maana ameanza kwa kasi kibarua chake akiwa na Simba, ili kuhakikisha anamshawishi kocha aendelee kumtumia kwenye kikosi chake cha kwanza.
Kama mchezaji huyo ataendelea kucheza kwa kiwango hicho anaweza kuhatarisha kibarua cha Mavugo ambaye katika mchezo wa jana aliushuhudia akiwa benchi kwa dakika zote 90 .
Simba imemsajili mshambuliaji huyo kwenye dirisha dogo akitokea Stand United ya Shinyanga na dhidi ya JKT Ruvu alionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kuwasahau mashambuliaji wa kimataifa Laudit Mavugo raia wa Burundi na Fredrick Blagnon raia wa Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment