Simba na Yanga zimekuwa na upinzani wa muda mrefu sasa kuanzia ndani na nje uwanja kwa miaka takribani 80 sasa tangu kuanzishwa klabu hizi na hakuna klabu hata moja itapenda kumuona mwenzake akifanikiwa uwanjani na nje ya uwanjani
Ni mara chache sana tofauti na miaka ya nyuma kwa klabu hizi mbili kuuziana wachezaji wao nyota kwa miaka ya 90 kurudi nyuma ila kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000 kuja mbele imekuwa ni jambo la kawaida kwa wanadinga hawa kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Ungana na makala hii Goal inakuchambulia wachezaji 11 bora walio wahi kukipinga kwenye klabu za Simba na Yanga kuanzia miaka ya 2000 hadi 2016
1.Juma Kaseja
Baada kuwa na kiwango bora ndani ya Simba kwa miaka 10 mlinda mlango huyu aliamua kupindikia upande wa pili mtaa wa Jangwani mwaka 2009 alicheza msimu moja pale kisha kurudi msimbazi kabla ajarejea tena yanga 2013
2.Hassan Kessy
Licha ya usajili wake kukumbwa na sintofahamu nyingi hadi leo, beki huyu wa kulia alifanya kazi nzuri Simba kabla ajageukia upande wa pili wa wapinzani
3.Amir Maftah
Mlinzi bora wa kushoto kuanzia miaka ya 2003 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2010 aliweza fanya kazi nzuri kwa timu zote kwa vipindi tofauti alikuwa bora kwenye ulinzi pia kuanzisha mashambulizi
4.kelvin Yondani
Wengi umfananisha na mlinzi wa zamani wa Manchester United Memanja Vidic hasa kutokana uimara wao wa kuzuia washambuliaji watukutu baada ya maisha mazuri ndani ya Simba kisiki huyu aliamua kukimbilia yanga miaka 4 nyuma na ndiyo klabu ambayo amepata mafanikio kuliko huko nyuma
5.Nurdin Bakari
Alipata jina ndani ya Yanga kwa miaka 7 kabla ajatua Simba kwenda kumaliza kiwango chake, Bakari ana uwezo wa kucheza kwenye namba mbali mbali
6.Athuman Idd
Alijiunga na Simba akitokea CDA ya Dodoma baada ya msuguano mkali na viongozi wa Mnyama kiungo huyu bora aliamua kusaini na Yanga, chuji ni moja ya viungo bora kuwahi kutokea hapa nchini
7.Mrisho Ngassa
Ngassa amecheza kwa mafanikio makubwa Jangwani kwa miaka yote aliyoitumikia amecheza Msimbazi kwa msimu moja tu kabla ya kurudi tena Yanga
8.Mohamed Banka
Banka amevitumikia timu zote hizi kwa kiwango bora, kiungo huyu fundi wa mpira alifanikiwa kuvuna mafanikio kwenye klabu zote hizo
9.Amiss Tambwe
Kati ya washambuliaji ambao Simba itawajutia kumpeleka kwa mtani wake basi ni Mrundi Tambwe rekodi zake ziko wazi tangu ajiunga na Yanga
10.hamis kiiza
Maarufu kama Diego, Mganda huyu mwenye rekodi nzuri ya ufungaji anakipiga kwenye Ligi Kuu ya Afrika ya Kusini alifukuzwa na Yanga na kuja kuibuka shujaa ndani ya sSmba msimu uliopita
11.Amri Kiemba
Baada ya kutupiwa virago Jangwani kutokana na kushuka kiwango chake kiungo huyu alkuja kuwa mmoja wa nyota bora nchini ndani ya klabu ya Simba sababu ya kiwango kikubwa alicho onesha Msimbazi
0 comments:
Post a Comment