Mwaka unakwisha vizuri kwa Cristiano Ronaldo baada ya kufikisha goli la 500 ukiwa ni muda mchache tangu alipotwaa tuzo ya Ballon d'Or
Katika ushindi wa leo Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Club America, mshindi wa Ballon d’Or, nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ametupia goli lake la 500 kwa klabu yake.
Wakikutana na Club America katika uwanja wa kimataifa wa Yokohama kwenye nusu fainali ya michuano hiyo, Los Blancos walishinda kwa mabao mawili kwa bila magoli yakipatikana kupitia Karim Benzema na Cristiano Ronaldo aliyefunga dakika za majeruhi.
Wakati klabu hiyo ikitinga fainali kucheza dhidi ya Kashima Antlers, CR7 binafsi amesherehekea goli lake la 500 tangu alipotua Real Madrid.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 31 tayari alikuwa ameshafikisha magoli 500 kwa klabu na nchi yake katika goli alilofunga Ureno dhidi ya Malmo hapo awali Septemba 2015 na alitimiza idadi hiyo akiwa amecheza mechi 753 tu. Lakini sasa akiwa amecheza mechi 689 Real Madrid tayari ametimiza magoli 500.
Pamoja na magoli 118 ya Manchester United katika mechi 292, magoli matano katika mechi 31 akiwa Sporting Lisbon, rekodi yake Real Madrid inasimamia magoli 377 katika mechi 367.
Takwimu hizo zinamfanya kuendelea kuwa mchezaji wa pili kufunga magoli mengi La Liga akiwa amefunga magoli 270 katika mechi 247, akiwa wa pili kwa nyota wa Barcelona Lionel Messi mwenye magoli 321 katika mechi 359.
Benzema: “Zidane ni kama kaka yangu”
Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema amedai kuwa meneja Zinedine Zidane ni kama kaka kwake.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amecheza mechi 11 tu za La Liga msimu huu, ambapo tatu aliingia kutokea benchi.
Benzema alikabiliwa na lawama katika kamepni, lakini amefanya kazi njema katika mechi ya Real Madrid Kombe la Dunia la Klabu ambapo walishinda dhidi ya Club America kutinga fainali.
Mshindi wa Ballon d’Or Cristiano Ronaldo aliisaidia timu yake kushinda kwa kufunga goli lake la 500 kwa miamba hao wa Hispania.
Baada ya mechi, Benzema alikiambia Teledeporte: “[Zidane] ni kama kaka kwangu. Ni mfano kwangu na ninafurahi kufanya naye kazi.
“Haukuwa mwaka mgumu kwangu, nimecheza vizuri katika mechi mbili au tatu. Umekuwa mwaka mzuri sana, ambao nimetwaa mataji na Real Madrid na kufunga magoli mengi.”
Benzema amefunga magoli manne ya ligi msimu huu na amefunga idadi hiyo hiyo pia kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.