ZAIDI kaya 98 katika Kitongoji cha Kirando na
Nyamamba wilayani ya Uvinza Mkoa wa Kigoma
hazina makazi ya kuishi mara baada ya mto
Kirando kujaa kutokana na mvua kubwa
iliyonyesha majira ya usiku hadi asubuhi.
Wakizungumza na waandishi wa habari wahanga wa
tukio hilo pamoja na viongozi wa kata
wamesema mvua hiyo ilianza kunyesha majira ya
saa sita usiku na kusababisha mto Kirando
unaomwaga maji yake Ziwa Tanganyika kujaa na
maji hayo kuingia katika makazi ya wananchi.
Aidha wameiomba serikali na wananchi
kuwapatia misaada ya chakula na maeneo ya
makazi ili waweze kujihifadhi wao na familia zao
ambapo mto huo imeelezwa ni kwa mara ya
kwanza kujaa na kusababisha madhara kwa
wananchi hao.
Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mrisho Gambo
ametoa wito kwa viongozi wa serikali ya Kijiji
kuzingatia na kuheshimu sheria za nchi ili
kuepusha majanga yanayo jitokeza kwa wananchi
wanaoishi kandokando ya vyanzo vya maji.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment