Comments


MWAMUZI PAMBANO LA WATANI WA JADI AWEKWA HADHARANI/TFf

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Tff
limemtangaza Mwamuzi mwanamama Jonesia
Rukyaa kuwa mwamuzi wa kati kwenye pambano
la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga,
mchezo utakaopigwa mwishoni mwa juma hili
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Aidha mwamuzi huyo mwenye beji ya FIFA
atasaidiwa na Josephati Bulali kutoka Tanga
pamoja na Samweli Mpenzu mkazi wa Arusha,
mwamuzi wa akiba anatarajiwa kuwa Elly Sasii
wa Dar es Salaam huku kamisaa wa mchezo huo
akiwa Khalid Bitebo wa Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
makao makuu ya TFF afisa habari wa shirikisho
hilo Baraka Kizuguto amesema maandalizi
kuelekea mchezo huo yamekamilika hivyo
akiwasihi wadau pamoja na mashabiki wa soka
kujitokeza kwa wingi kununua tiketi kwa ajili ya
mchezo huo ambazo zitaanza kuuzwa rasmi
majira ya saa mbili asubuhi siku ya ijumaa.
Kizuguto ametaja pia viingilio vya mchezo huo
kuwa Shilingi 7000 kwa viti vya Blue na Kijani,
elfu 10, kwa viti vyenye rangi ya Machungwa,
shilingi elfu 20 kwa VIP B na C, huku viti vya VIP
A vikiwa shilingi elfu 30.
Sambamba na mechi hiyo ya simba na yanga,
kuna michezo mingine itakayopigwa siku hiyo
ambapo Mbeya City watacheza na Azam katika
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United
itacheza na JKT Ruvu uwanja wa Kambarage
mjini Shinyanga, Toto Africans na Kagera Sugar
CCM Kirumba jijini Mwanza, Mgambo Shooting
dhidi ya Tanzania Prisons katika Uwanja wa
Mkwakwani Tanga, n Majimaji fc wao wakiwa
wageni wa Mtibwa katika uwanja wa Majimaji
mjini Songea.
Ligi hiyo pia itaendelea siku ya jumapili kwa
michezo miwili ambapo Mwadui FC dhidi ya
Coastal Union kwenye uwanja wa Mwadui
Complex, na Ndanda FC watacheza na African
Sports uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system